WQNAFUZI 106 WASITISHA MASOMO KWA KUPATA UJAUZITO
Ukerewe. Wanafunzi 106 wa shule za msingi na sekondari wilayani hapa wamefukuzwa baada ya kubainika kuwa na ujauzito, wakati wa upimaji uliofanyika kati ya Januari na Aprili.
Katibu tawala wilaya ya Ukerewe, Focus Majumbi alisema kati ya wanafunzi hao, wawili ni wa shule za msingi huku waliosalia wakiwa ni wa sekondari.
“Sekondari ya Ilugwa iliyopo kisiwani, pekee ilikutwa na wanafunzi 11 wenye mimba,” alisema na kwamba, tayari wanaume 28 waliodaiwa kuwapa ujauzito wanafunzi hao wamefikishwa mahakamani.
Ili kukabiliana na tatizo la mimba shuleni, wilaya imeweka mikakati ikiwamo kupiga marufuku matamasha ya muziki nyakati za usiku maarufu Mazinduke.
Naye mkuu wa Sekondari ya Ilugwa, Emmanuel Bomba alisema kati ya wanafunzi 11 waliobainika kuwa na ujauzito shuleni kwake, mmoja alipewa ujauzito na mjomba wake. Alisema kati ya wanafunzi 283 wa shule hiyo yenye mabweni mawili yanayochukua wanafunzi 96 kila moja, ni kumi pekee wazazi wao wamewalipia Sh480,000 za chakula na malazi. Shule hiyo iliyoko kwenye moja ya visiwa 38 vya Ukerewe, inapokea wanafunzi kutoka visiwa vya Kulazu na Buluza.
Kuhusu mikakati hiyo, ofisa elimu sekondari wilaya, Venance Nyamwale alisema Serikali inafanya jitihada kukabiliana na changamoto zinazokwamisha maendeleo ya wanafunzi wa kike
Comments
Post a Comment