Akifanya Gurdiola ni fresh tuu ila akifanya Mourinho ni noma
Nimekumbuka msemo wa Wazaramo baada ya jana kumuona Mhispania Pep Gurdiola ambaye wiki chache tu zilizopita alitupiwa shutuma kwamba hana nidhamu na jana tena akaionesha dunia kwamba ana mihemko iliyopitiliza.
Unakumbuka wakati Jose Mourinho akiwa katika eneo lake na akapiga kopo la maji baada ya kuona Pogba amepewa kadi kwa uonevu wakati wa mechi zidi ya West Ham? Refa hakufikiria mara mbili zaidi ya kumpa adhabu akaenda jukwaani.
Achana na faini ambazo amekuwa hazikosi kila baada ya muda kadhaa lakini FA mara nyingi wamekuwa wakimmulika Mourinho na vitu vingi afanyavyo wamekuwa hawamuacho salama, kama sio onyo ni adhabu.
Jana kumejitokeza tukio ambalo hii leo limekuwa mjadala mkubwa duniani baada ya Pep Gurdiola kupita eneo lake na kumfuata mchezaji Nethan Redmond na kuonekana wazi wazi kwamba alikuwa akimbughuzi baada ya goli la dakika ya mwisho la Raheem Sterling.
Video zinaonesha Gurdiola akimshika Redmomd nyuma ya kisogo, akirusha mikono na kumuangalia kwa ghadhabu jambo ambalo watu wengi wamelitafsiri kwa maoni tofauti lakini wengi wakimshangaa Pep na kuuliza hivi ndivyo inavyopaswa kuwa ukipata goli dakila za majeruhi?
Hadi sasa shirikisho la soka nchini Uingereza FA halijalisemea tukio hilo na hakuna dalili yoyote ya tukio la Gurdiola kuchukuliwa hatua na hii imeanza kuleta maswali na swali kubwa ikiwa, kama Mourinho au Conte angefanya kitendo kile angekuwa salama?
Upande wa pili unadai Pep ni kocha mpole asiyependa kuzungumzia waamuzi na timu nyingine kama Mourinho, lakini sheria ni sheria haijalishi wewe unasemaje au wewe unaongea nini lakini ukifanya kosa wote munaadhibiwa.
Haipo katika sheria lakini kuna nyakati soka linazuia kufanya kitendo cha kumuudhi,kumdhalilisha au kumbughudhi mpinzani wako na ndio maana msimu wa mwaka juzi Neymar alioneshwa kadi ya njano baada ya kucheza chenga ilionekana kutaka kumdhalilisha mlinzi wa timu pinzani wakati Barca wakiwa wanaongoza.
Muandishi mmoja nguli wa michezo katika makala yake amehoji kuhusu mhemko wa Pep jana una funzo gani kwa vijana wadogo ambao waliangalia mpira? Ina maana timu yako ikishinda goli dakika za mwisho ndio uwafanyie wapinzani vile?
Na hata hivyo Pep pamoja na ustaarabu wake lakini mara kadhaa ameonekana akikosa nidhamu mbele ya wapinzani na hii ndio sababu ya Maurcio Pochettino kumuita “asiye na nidhamu” baada ya kuawaita Tottenham “THE HARRY KANE TEAM”
Pep hatafungiwa na FA, Pep atasifiwa na wengine watasema ni sawa tuu kwanza hajazoea kufanya hivyo pia atakuwepo katika Manchester Derby wiki ijayo na hapo ndio tutarudi kwa wazaramo tena wanaposema “SEMA WEWE MIRINDA (GURDIOLA) NIKISEMA MIMI PEPSI(MOU) NAAMBIWA NINA GESI
Comments
Post a Comment