Kumbe Dk Shika anajuana na Abromovich, ni shabiki wa Chelsea
Yule ' Bilionea wa nyumba za Lugumi' Dk Louis Shika ambaye hivi
karibuni alisema kuwa ni shabiki wa Chelsea kwa kuwa mmiliki wa klabu
hiyo, Roman Abramovich ni rafiki yake, amefafanua zaidi.
Shika ambaye kitaaluma ni Daktari amesema kwamba, alikuwa akikutana na Abramovich mara kadhaa katika mikutano ya wadau.
Amesema kwa kuwa yeye ni mmiliki wa kampuni ya masuala ya kilimo, walikuwa wakikutana na Abramovich mara kwa mara katika mikutano ya viwanda.
“Mimi nilikuwa ninashughulika na masuala ya kilimo na yeye masuala ya mafuta. Sasa kule Urusi kuna kawaida ya makampuni kukutana.
“Kunakuwa na mikutano ya kuwakutanisha wamiliki kujadili mambo mbalimbali. Unajua kilimo pia kinahitaji mafuta na wauza mafuta wanawahitaji watu wa kilimo na makampuni mengine. Sasa pale nilikuwa ninakutana naye (Abramovich).
“Niliposikia kuwa yeye ndiye mmiliki wa Chelsea, basi nikaanza kuifuatilia na mwisho nikawa naipeda,” alifafanua.

Comments
Post a Comment