Chirwa, Okwi, bampa to bamba

Hat-trick ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa ni ya pili kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya Emanuel Okwi kufanya hivyo (Okwi alifunga goli 4) kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi August 26, 2017 Simba ilipocheza dhidi ya Ruvu Shooting.

Chirwa amepiga bao tatu wakati Yanga ikipata ushindi wa goli 4-0 kwenye uwanja wa Uhuru dhidi ya Mbeya City.

Mabao matatu aliyofunga leo Chirwa yanamfanya amfikishe magoli sita (6) na kumfikia mshambuliaji Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons.

Emanuel Martin alifunga magoli mengine mawili kukamilisha idadi ya magoli 5-0.

Mbeya City wameendeleza rekodi yao ya kufungwa na Yanga kila wanapocheza Dar. Tangu imepanda kucheza ligi kuu Tanzania bara timu hiyo ya mkoani Mbeya imefungwa mechi zote tano ilizocheza dhidi ya Yanga kila ipocheza Dar.

2013/14 Yanga 1-0 Mbeya City
2014/15 Yanga 3-1 Mbeya City
2015/16 Yanga 3-0 Mbeya City
2016/17 Yanga 2-1 Mbeya City
2017/18 Yanga 5-0 Mbeya City

Magoli 5-0 ni ushindi wa kwanza mkubwa kwa Yanga katika mechi tano ilizocheza kwenye uwanja wa Uhuru.

Yanga 1-1 Lipuli
Yanga 1-0 Ndanda
Yanga 0-0 Mtibwa Sugar
Yanga 1-1 Simba
Yanga 5-0 Mbeya City

Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Mbeya City msimu huu wakiwa wamecheza mechi 10 hadi sasa. Pia ni kipigo chao cha kwanza kikubwa tangu imeanza kucheza na Yanga (kipigo kikubwa kilikuwa Yanga 3-0 Mbeya City

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya