Kim Jong Un: Marufuku pombe na muziki Korea Kaskazini



Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amepiga marufuku mashirika ya burudani yakiwemo yale ya pombe na muziki.

Kwa mujibu wa habari,Korea Kaskazini imefanya hivyo kwa nia ya kudhibiti uchumi wa nchi hiyo hasa baada ya vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa mataifa,

Korea Kaskazini imewekewa vikwazo vingi kutokana na kukiuka masharti na kuendelea kutengeneza makombora ya nyuklia.

Wananchi nchini humo wamekuwa wakijaribu kuishi ndani ya matakwa ya serikali.

Mbali na kuwa vigumu kwa wananchi wa Korea Kaskazini kusafiri nje ya nchi,utumiaji wa mitandao ya kijamii bila idhini ya serikali nao umedhibitiwa vilivyo.

Hata hivyo Pyongyang haionyeshi dalili zozote za kaucha kufanya majaribio ya makombora ya nyuklia

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya