Fanya hivi kujitibu ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo

 

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo kwa miaka ya hivi karibuni  umekuwa ni tishio, huku wengi wakiwa hawaelewi wafanye nini ili kujitibu, hivyo kutokana na tatizo  hilo wengi wamekuwa wakipoteza matumaini ya kwamba ugonjwa huo hauna tiba, kama ndivyo hivyo na endapo unasumbuliwa na ugonjwa huo unashauriwa kutumia vitu vifuatavyo ili uwweze kupona ugonjwa huo.

1. Ndizi mbivu
Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo ‘H. Pylori’.
Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo.

Nini cha kufanya;

  • Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula walau ndizi zilizoiva 3 kwa siku.
  • Au menya ndizi 2 au 3 na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa. Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa wiki 2 hivi.


2. Kabeji
Kabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.

Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U ambavyo ni muhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.

Nini cha kufanya;

  • Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.
  • Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.
  • Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.


3. Nazi
Nazi ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. Nazi huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la nazi na maji ya nazi (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.
  • Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la nazi au maji ya nazi kila siku. Pia unaweza kuitafuana nazi yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki 2 ili kupata matokeo chanya.
  • Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki 2 hivi
BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA DALADALA YA G.I.B Carter.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya