ALICHO KISEMA LWANDAMILA BAADA YA TAMBWE KUREJEA MAZOEZINI


WAKATI keshokutwa wakijiandaa kuwakabili Mbeya City, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amewataka wachezaji wake kuweka nidhamu mbele ndani na nje ya uwanja ili kufikia malengo yao.

Lwandamina, ambaye anaonekana kuwa mkimya na asiyependa kuongea sana, amesema anataka kuona kila mchezaji anatimiza majukumu yake na kufuata kile anachoelekezwa na makocha wa timu hiyo.

Alisema mchezo dhidi ya Mbeya City ni mgumu na ili waweze kushinda lazima wawaheshimu wapinzani wao hao.

“Tunaenda kukabiliana na timu nzuri ambayo inawachezaji wenye uzoefu, Yanga ni timu kubwa lakini wachezaji lazima wawaheshimu wapinzani wetu na kucheza kwa kujituma ili kufikia malengo yetu ya ushindi,” alisema Lwandamina.

Aidha, alisema kuwa amefurahi kuona mshambuliaji wake, Amissi Tambwe akirejea mazoezini na hilo litaongeza nguvu kwenye kikosi chake.

“Tambwe ni mchezaji muhimu, kurejea kwake kutatuongezea nguvu, tunaye Ajibu (Ibrahim) na Chirwa (Obrey) kwenye safu ya ushambuliaji na wanafanya vizuri, kurejea kwa Tambwe kutaongeza kitu,” alisema kocha huyo.

Alisema anaweza asimtumie kwenye mchezo wa Jumapili lakini kama ataendelea vizuri anaweza akamtumia kwenye mchezo mwingine utakaofuata dhidi ya Tanzania Prisons ambao utafanyika Novemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru.

Tambwe hajacheza mchezo wowote tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na kuwa majeruhi lakini wiki hii mshambuliaji huyo fundi wa kuzifumania nyavu ameanza mazoezi na kuleta matumaini mapya kwa mashabiki wa timu hiyo

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).