MGOSI:Heshima yako Chirwa


MGOSI

Mshambuliaji nyota wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mussa Hassan Mgosi, amesema kuwa kwenye Ligi Kuu Bara mshambuliaji mbishi uwanjani ni Obrey Chirwa wa Yanga.

Chirwa ambaye amekuwa tishio katika kufunga, mpaka sasa ana mabao sita yakiwa mawili nyuma ya anayeongoza ambaye ni Emmanuel Okwi wa Simba.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Global TV Online, Mgosi alisema hata akichezewa faulo bado mchezaji huyo amekuwa hakati tamaa kiasi cha kuwafanya mabeki wengi kumuogopa.

“Enzi zangu mimi hata ukinichezea rafu vipi, ndiyo kwanza nakuja kwani straika ukigongwa kidogo halafu ukahama upande unampa kichwa yule beki kuwa kakuweza.

“Katika ligi kuu, kwa sasa straika nunda ni Chirwa kwani ndiye namuona hata ukimchezea rafu vipi bado atakufuata, mwingine ni John Bocco,” alisema Mgosi.

Mgosi alikuwa mmoja wa washambuliaji matata na wasumbufu wanapokuwa uwanjani.

Mshambuliaji huyo aliyetokea Mtibwa Sugar kutua Simba, alikuwa akihofiwa sana na mashabiki wa Yanga kipindi timu hizo zinapokutana.


Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya