Utata mwingine waibuka kwa 'Tajiri' Dkt. Shika

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limedai kuwa lina mashaka kuhusu uhalali wa udaktari wa mtu mmoja anayedaiwa kuwa Tajiri  aliyeshinda katika mnada wa kuuza nyumba za mfanyabiashara Lugumi uliofanyika juzi siku ya Alhamisi kwa kuwaameshindwa kuonyesha vielelezo kuthibitisha elimu yake ya kiwango cha Ph.D

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amesema wanaendelea na upelelezi dhidi ya mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Dkt. Louis Shika na kwamba jana hiyo walikwenda kumkagua nyumbani kwake Tabata Mawenzi.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa  Shika hana taaluma ya udakatri na kwamba inasemekana huenda alitumwa na Mfanyabiashara Lugumi mwenyewe kuharibu mnada huo baada ya kushindwa kutoa fedha ambazo alidai ziko nje ya nchi.

“Tulipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart, Stanley Kevela, kuwa huko Mbweni JKT wakiwa wanafanya mnada wa hadhara wa kuuza nyumba za mfanyabiashara Lugumi, alijitokeza mtu anayeitwa Shika ambaye alishinda mnada huo kwa kutaka kununua nyumba zote tatu, kumbe hakuwa na fedha,” alisema Mambosasa.

Mambosasa alisema '‘tajiri’ huyo alitaka kununua nyumba moja ya Mbweni kwa Sh. bilioni 1.2, nyumba ya pili iliyoko pia Mbweni Sh. milioni 900 na nyumba ya tatu iliyoko Upanga alishinda na kutaka kununua kwa Sh. bilioni 1.2 na  Mtuhumiwa huyo alitakiwa kulipa asilimia 25 ya fedha kwa kila nyumba lakini hakuwa na fedha ndipo walipomkamata na kumfikisha kituo cha polisi kwa hatua zaidi.

Aidha, Kamanda Mambosasa alisema taarifa zinaonyesha kuwa inawezekana Mtu huyo alitumiwa na Mfanyabiashara Lugumi mwenyewe kwa kuwa alivyotakiwa kutoa fedha alisema ziko nchini Russia na Lugumi hajulikani mahali anapoishi kwa sasa.

 Pia alisema wanaendelea kumhoji juu ya taaluma ya udaktari aliyoitaja ingawa bado alikuwa hajaithibitisha kwa kutoa vielelezo.

“Amesema ni daktari lakini hajathibitisha kwa hiyo udaktari wake hadi sasa ni wa madai, hivyo amefanya kazi wapi hajatuambia.  Upelelezi unaendelea na atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya