Mbeya City Yalazimika Kufanya Mabadiliko ya Dharura
Klabu ya soka ya Mbeya City imelazimika kubadili jezi yake iliyokuwa imepanga kuitumia kwenye mechi ya ugenini leo dhidi ya Singida United.
Mbeya City imefikia uamzi huo baada ya kuwepo kwa mfanano kati ya jezi yake ya Singida United ambao ni wenyeji wao katika mchezo wa leo.
Jezi hizo ni kama zinavyoonekana hapo chini ambapo kushoto ni jezi ya wenyeji Singida United na kulia ni jezi ya Mbeya City iliyokuwa imepangwa kutumika leo.
Hata hivyo bado Mbeya City hawajasema ni jezi gani ambayo watatumia lakini msimu huu jezi zao za pili kwaajili ya mechi za ugenini ni zile zenye rangi ya damu ya mzee hivyo huenda ndio zitakazotumika leo.
Singida United inayoshika nafasi ya 5 ikiwa na alama 17 inacheza leo na Mbeya City yenye alama 11 katika nafasi ya 10 kwenye mchezo wa raundi ya 11, uwanja wa Namfua mjini Singida

Comments
Post a Comment