Robert Mugabe Agoma Kula...Apania Kufa Akiwa Rais



Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe inasemekana amekuwa akikataa kula na kuzungumza kwa siku kadhaa sasa akiwa amepania ‘kufa kwa ajili ya jambo sahihi’ wakati amewekwa chini ya ulinzi nyumbani kwake.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza limesema mpwa wa kiongozi huyo aitwaye, Patrick Zhuwao, alisema Jumamosi kwamba Mugabe yuko tayari kufa akipigania kile anachokiita ni sahihi.

Habari zingine kutoka nchini humo zinasema chama tawala cha ZANU-PF kitamwondoa Mugabe kwenye uongozi katika mkutano maalum unaotarajiwa kufanyika leo Jumapili. Mkutano huohuo unatarajiwa kumrudisha aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Munangagwa, ambaye alifukuzwa na Mugabe wiki mbili zilizopita.

Vilevile kuna uvumi kwamba kiongozi huyo ameikimbia nchi hiyo baada ya mamia ya maelfu ya watu kuandamana kupinga utawala wake. Waandamanaji hao walionekana wakichana matangazo yaliyo nje ya makao makuu ya Zanu-PF yakimwonyesha Mugabe.

Hata hivyo, Mugabe anategemewa kuzungumzia hatima ya kuondoka kwake madarakani na mkuu wa majeshi Constantine Chiwenga ambaye alimweka kizuizini nyumbani kwake.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya