“Mara Nyingi Nilitamani Kujiua” Emmanuel Adebayor
Emmanuel Adebayor amekuwa mwanasoka ambaye ametawaliwa na matukio mengi
sana nje ya uwanja, Adebayor amekuwa na maisha magumu ndani ya uwanja na
mara zote amekuwa akiishutumu familia yake.
Mara kadhaa Adebayor amekuwa akidai kwamba chanzo cha yeye kuwa na kiwango kibovu uwanjani ilikuwa ni uchawi anaofanyiwa na ndugu zake. Adebayor alishawahi kwenda mbali kwa kudai kuwa mama yake alimchongea atimuliwe Madrid.
Sasa Emmanuel Adebayor ameibuka na jipya ambapo anasema familia yake ilimchanganya kiasi cha kumfanya kujaribu kujiua mara kadhaa, Adebayor anadai familia ilimpa msongo wa mawazo wakati wote.
Familia ya Adebayor ambayo inaishi nchini Togo ni maskini sana na wanatajwa kwamba walikuwa wakihitaji kiasi kikubwa cha pesa kutoka kwa mwanasoka huyo kiasi cha kutumia mbinu nyingi ili wazipate.
“Nilitamani kujiua mara nyingi tuu na hili nilikuwa silisemi kwa mtu na nimekaa nalo kwa muda mrefu, sikutaka kuliongea jambo hili lakini sasa naona kama kulisema hadharani itanisaidi kuwa huru” alisema Adebayor.
Adebayor anasema amekuwa akizungumza na mdogo wake mara nyingo kuhusu familia yake inavyomfanyia kiasi cha kufikia kuamua kubadili namba ya simu ili kuwafanya wasiwe wanamtafuta.
Adebayor anasema kati ya sababu kubwa iliyomfanya kubadili namba ya simu ni tukio la familia yake kumpigia simu wakati akiwa majeruhi na kumuomba pesa bila hata kumuuliza anaendeleaje.
Ukiachana na dada yake Adebayor amekuwa akiamini kikwazo kikubwa kwake ni mama yake mzazi ambapo wakati akiwa Tottenham alisema wazi kwamba kiwango kibovu kilitokana na ndumba za mama yake.
Baada ya kuachana na Crystal Palace, Adebayor alikaa nje kwa muda mrefu akiwa hana timu ya kuichezea lakini sasa yuko nchini Uturuki katika klabu ya Istanbul Basksehir.

Comments
Post a Comment