WAJEDA’ WAMUONYA CHIRWA




MABEKI wa timu ya Tanzania Prisons wamemuonya straika wa Yanga, Obrey Chirwa, kuwa asitarajie mteremko alioupata kwa Mbeya City, pindi watakapokutana kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Prisons inashuka dimbani ikiwa imetoka kupoteza nyumbani dhidi ya Simba kwa kufungwa bao 1-0, huku Yanga wakiwa bado na furaha ya ushindi wa mabao 5-0 walioupata dhidi ya Mbeya City.

Wakizungumza baada ya mazoezi ya juzi jioni katika Uwanja wa Chuo cha Magereza, Ukonga, mabeki hao, Laurian Mpalile na Salum Kimenya, walisema wanajua ubora wa Chirwa hivi sasa, hivyo wamejipanga kukabiliana naye.

“Mchezaji anapokuwa katika kiwango kikubwa kama Chirwa lazima umpe heshima yake, lakini si kumuogopa anapokuwa mpinzani wako, sisi   tumejipanga kupambana na kuibuka na ushindi,” alisema Kimenya.

Kwa upande wake Mpalile, alisema kama Yanga waliwaweza Mbeya City na mchezaji wao Chirwa kufunga hat-trick, wajipange zaidi kukabiliana na safu ya ulinzi ya Prisons, kwa kuwa hawapo tayari kupoteza tena mchezo wa pili.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Prisons ipo nafasi ya sita na pointi 14 kwa kucheza mechi 10 na kushinda tatu, sare tano na kupoteza mbili.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya