HABARI IN! Ile ishu ya MAVUGO kutimukia Yanga yapamba moyo.


Mshambuliaji Laudit Mavugo hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba na yupo mbioni kuachwa, Yanga imeelezwa kukamata fursa na kutaka kufanya kama ilivyokuwa kwa Amissi Tambwe.



Desemba 2014, katika msimu wa Ligi Kuu Bara wa 2014/15, Simba ilimtema Tambwe ikiamini amekwisha lakini Yanga ikamsajili fasta na akashika nafasi ya pili ya ufungaji akiwa na mabao 14.

Sasa Yanga inasubiri Simba impe barua ya kumuacha Mavugo raia wa Burundi ili imnase na kumpa mkataba mpya kama mambo yataenda sawa kwani ina mipango mingi inafanya.

Bosi mmoja wa Kamati ya Usajili ya Yanga, amesema wana mpango wa kumuacha mmoja kati ya washambuliaji wake ama Donald Ngoma au Tambwe halafu wasajili straika mmoja wa kigeni.

“Mmoja kati ya Tambwe au Ngoma tutamuacha kutokana na majeraha yao, ila katika usajili tunaangalia nje ya nchi lakini tunaisikilizia Simba kama itamuacha Mavugo, sisi tutamchukua.

“Lakini hii itawezekana endapo Simba itakubali kuachana naye jumla Mavugo kwani hawataweza kumleta kwa mkopo kwetu, unajua tunataka kufanya kama ilivyokuwa kwa Tambwe,” alisema bosi huyo.

Alisema wanaamini Mavugo akipata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu anaweza kuwa tishio kwa ufungaji kwani Simba hawampi nafasi hiyo kaam ilivyokuwa kwa Tambwe mwanzoni ma msimu wa 2014/15.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa hakuwa tayari kusema chochote kuhusu zaidi kusema wanasubiri ripoti ya kocha wao, George Lwandamina ndipo waanze harakati za kukiimarisha kikosi chao.

Naye Mavugo alipoulizwa kuhusu mpango huo wa Yanga, naye hakuwa tayari kusema lolote akisema bado ana mkataba na Simba hivyo kuzungumzia
kwenda popote


TAZAMA PIA VIDEO YA KUMBUKUMBU YA ASLAY '' TIGO FIESTA''kwa mara ya kwanza Iringa. 

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).