Uchambuzi wa Wimbo Mpya wa Diamond Platnumz Unaitwa Sikomi


UCHAMBUZI WA WIMBO
JINA LA WIMBO: SIKOMI
MSANII : DIAMOND PLATNUMZ

UTANGULIZI

Diamond Platnumz ni msanii wa muziki wa kizazi kipya (bongofleva) kutoka Tanzania. Anaiwakilisha nchi yake na fasihi ya kiswahili nje na ndani ya nchi kwa ufanisi. Wimbo wake mpya wa Sikomi ni mojawapo ya nyimbo zake nyingi ambazo amepata kuziimba tangu alipoanza mziki wake. Ufuatao ni uchambuzi wa wimbo wa Sikomi. Angalizo uchambuzi huu utajikita zaidi kwenye vipengele vya maudhui na wala mhakiki hajagusa vipengele vya fani.

DHAMIRA KUU
Dhamira kuu katika wimbo wa Sikomi ni mapenzi. Msanii anaeleza historia yake ya kimahusiano toka alipotoka kimuziki mpaka hapa alipofika. Amegusia visa na mikasa aliyopitia katika mahusiano yake ya kimapenzi. Msanii amepitia katika mengi katika mapenzi lakini bado haachi kujihusisha na mapenzi huu ndiyo msingi wa jina la wimbo "Sikomi". Msanii anasema kila anapoumizwa na mwanamke mmoja anatafuta mwanamke mwingine wa kumfuta machozi.

DHAMIRA NDOGO NDOGO

USALITI KATIKA MAPENZI

Msanii anaeleza jinsi alivyosalitiwa na wanawake aliowapitia msanii anasema " aliyonifanyia wa sentro siwezi Sema... ndiyo maana sikushangaa ile ghafla toka CCM kwenda CHADEMA"
Msanii anaeleza jinsi alivyoumizwa na usaliti katika mapenzi. Msanii anasema mara baada ya kutoka kimuziki alivamia tasnia ya bongo movie ambapo alisalitiwa sana.

Msanii anaeleza jinsi alivyosalitiwa na Penny aliyedai ana ujauzito wake hali iliyompelekea kumhonga gari mpenzi wake huyo ambaye mwisho wa siku alikuja kumsaliti. Msanii anasema ameshafumania na kufumaniwa pia katika mapenzi hii ni kielelezo cha usaliti katika mapenzi kwenye kazi ya msanii.

MIGOGORO
Msanii amesadifu yale yanayotokea katika jamii kwa kuonesha migogoro mbalimbali kwa kutumia wahusika katika wimbo wake baadhi ya migogoro ni hii ifuatayo;

Mgogoro wa msanii na mama yake

Mgogoro wa nafsi wa msanii kuhusu kuachana na mapenzi au kuendelea.

Mgogoro wa msanii na Esma kuhusu kuachana na mapenzi ni baada ya Esma kumwambia msanii mapenzi basi msanii hakutaka kusikia.

Mgogoro wa msanii na Zari. Msanii anasema richa ya Zari kumzalia watoto wawili wa kiume na wa kike lakini bado alimsaliti.

Mgogoro wa Msanii na wa Sentro na mgogoro wa msanii na wa sentro.

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII

Msanii amemchora mwanamke kama mzazi na mlezi mfano ni mama yake na msanii na Zari.

Msanii amemchora mwanamke kama mshauri mzuri mfano ni mama yake na msanii na Esma.

Mwanamke kama mtu mwenye mapenzi ya dhati mfano Zari aliyempenda msanii mpaka kumzalia watoto wawili, mama yake msanii na Esma.

Msanii amemchora mwanamke kama mtu aliyekosa msimamo na msaliti, mfano wa Sentro na Penny.

KUFANIKIWA KWA MSANII KIMAUDHUI

Msanii ameweza kusawiri ipasavyo mambo yanayotokea katika jamii ya kitanzania na hasa katika ulimwengu wa mapenzi.

UDHAIFU WA MSANII
Msanii amekuja na hitimisho jumuishi kuwa wasanii wa sinema (bongo movie) siyo wa kuaminiwa jambo ambalo siyo la kweli kwenye uhalisia kwani kuna wasanii wengi wa tasnia ya filamu wanajiheshimu na wengine ni watu wazima wenye kujiheshimu pia na kuaminika na jamii. 

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya