WANAUME WAWE MBELE KUPIMA VVU
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wadau na Watumishi wa Sekta ya Afya katika siku ya uzinduzi wa Mwongozo wa kutoa cheti kwa maeneo ya kufanyia vipimo vya VVU katika vituo vya kutolea huduma za Afya. Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Ubora toka Wizara ya afya Dkt. Mohamed Mohamed akimkaribisha mgeni rasmi mapema leo katika siku ya Uzinduzi wa Mwongozo wa kutoa cheti kwa maeneo ya kufanyia vipimo vya VVU katika vituo vya kutolea huduma za Afya. Wadau wa masuala ya Afya wakifuatilia kwa ukaribu taarifa is juu ya Uzinduzi wa Mwongozo wa kutoa cheti kwa maeneo ya kufanyia vipimo vya VVU katika vituo vya kutolea huduma za Afya, tukio lililofanyika katika ofisi za NMRI jijini Da es salaam. Mwakilishi kutoka CDC Kevin De Cock akiwasilisha salamu kutoka CDC mbele ya Naibu Waziri...