Yanga yawaweka hadharani wachezaji wao wapya


Klabu ya Yanga imetangaza wachezaji wawili ambao wamesajiliwa katika dirisha dogo la usajili ambalo linafungwa kesho na kusema kuwa muda bado upo hivyo watu wasubiri mpaka muda ukapofungwa ndipo watajua kama kutakuwa na wachezaji wengine.

Msemaji wa klabu ya Yanga, Dismas Ten amewataja wachezaji hao walisajiliwa kuwa ni pamoja na Yohana Mkomola pamoja na Fiston Kayembe

"Wachezaji ambao wametangazwa mpaka sasa ni hao wawili ndiyo wamesajiliwa na Yanga, dirisha linafungwa kesho hivyo muda bado upo huwezi kujua nini kitatokea kwani kamati ya usajili bado inaendelea kufanya majukumu yake mpaka pale ambapo dirisha litakuwa limefungwa ila kwa sasa taarifa ambayo ipo ni kuhusu hao wachezaji wawili ambao tumewatambulisha kama wachezaji wapya wa Yanga" alisema Dismas Ten

Aidha Dismas Ten ameendelea kusisitiza kuwa kamati ya usajili inaendelea na kazi yake hivyo inawezekana wakatangaza jambo jingine kabla ya usajili kufungwa kesho

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya