HAKIKA AMEREJEA KAZINI

Na GODFREY MPAGIKE.
Hakika amerejea mshambuliaji mahiri wa Yanga HAMISI J TAMBWE. Ni mara baada ya kurejea kutoka katika majeraha sasa aanza rasmi kazi yake ya upachikaji mabao
Huu ni mchezo wake wa kwanza katika mashindano ukiachana na ule wa kirafiki ambao ulimalizika kwa timu zote mbili kutoshana nguvu
Leo 24/12/2017 katika mchezo wa FA cup Tambwe anafunga goli zuri la kichwa akimwacha kipa akijirusha kuokoa lakini mpira ukawa ushajaa kimiani
Si Tambwe tuu aliye ipatia ushindi timu hiyo ya mabingwa wa kihistoria mfululizo mara tatu ligi kuu Vodacom ni kijana mahiri Pius Buswita aliye piga shuti kali ambalo lilimshinda golikipa wa wapinzani REHA FC na kujaa katika kimia na kuifanya Yanga kuongoza dakika ya 81 ya mchezo baada ya Tambwe kukomelea tena goli la pili
Hakika yanga wameepuka dhahama iliyo weza kumkuta mtani wake SIMBA na kufanya mitaa ya jangwani kuwa na utulivu na kusherekea Krismas wakiwa na furaha tele.
Vijana wa REHA FC walijitahidi na kufanikiwa kufika langoni pa Yanga lakini walishindwa kukwamisha mpira kimiani kutokana na umahiri wa kipa wa yanga, hivo mpaka mpira unamalizika YANGA 2-REHA FC O.


Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya