Barnaba Classic Atangaza Kuachana na Mziki

Barnaba Classic Atangaza Kuachana na Mziki


Ikiwa zimebaki siku sita tu kabla ya kuumaliza mwaka 2017 na kuingia 2018, staa wa Bongofleva Barnaba Classic ametangaza kuwaaga mashabiki wake kwa mwaka huu na atakuwa kimya kimziki kwa muda.


Mkali huyo wa sauti na uandishi kwenye kiwanda cha mziki Bongo, ameweka wazi kuwa ukimya wake utaanzia kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na kujipanga namna ya kuuanza kwa kishindo mwaka 2018.

“Nikiwa najitoa kwenye mitandao ya kijamii kidogo, ningependa kuwatakia mashabiki, marafiki na familia yangu Heri ya Christmas na Mwaka Mpya”, amefunguka Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Pamoja na kujitoa kwake nyota huyo anayetemba na ngoma yake ya Mapenzi Jeneza ameongeza kuwa anajiweka vizuri kuanzia mwonekano mpaka sound ya hit zake zijazo.

“Ninapumzika kidogo ili kuweka mipango yangu vizuri kwaajili ya mwaka 2018. Nitawaletea Barnaba mpya mwenye kila jipya kimuziki na hata Sound” ameongeza

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya