Baada ya Kuzushiwa Kifo Haji Manara Awatoa Hofu Wapenzi Wake

Baada ya Kuzushiwa Kifo Haji Manara Awatoa Hofu Wapenzi Wake


Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amesikitishwa na taarifa za kuzushiwa kifo zilizosambaa mitandaoni wakati yeye ni mzima kabisa.


Haji Manara amesema yeye yupo hai akiwa na afya imara na anamshukuru Mungu huku akitoa pole kwa ndugu na jamaa ambao wamepata usumbufu kwa namna moja ama nyingine kutokana na taarifa hizo za uongo.

“Taarifa zinazoenezwa mitandaoni juu ya uhai wangu si kweli, nipo hai na mzima wa afya kwa uwezo wa Mungu, poleni nyote mliokuwa msibani kwa kupewa taarifa isiyo sahihi, poleni pia familia yangu.hususani mama na dada zangu”, ameandika Manara kupitia Ukurasa wake wa Instagram.

Haji Manara amejizolea umaarufu nchini kutokana na uhodari wake wa kutekeleza majukumu ya kazi yake kama msemaji wa Simba ambapo mara nyingi hutumia maneno ya utani kufikisha taarifa zake hususani zile zinazohusu wapinzani wao wakuu klabu ya Yanga SC.

Kitendo hicho cha kuzushiwa Kifo kimeonekana kuwakera wafuasi wake wengi ambao wametoa pole zao kupitia sehemu ya maoni (Comment) katika picha aliyoiweka kwenye mtandao wake.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).