SIMULIZI;Najuta kukufahamu OLIETER;SEHEMU YA KWANZA [1]

SEHEMU YA KWANZA 
SIMULIZI;NAJUTA KUKUFAHAMU OLIETER
MTUNZI  ; GODFREY JOHAKIM MPAGIKE
TEL          ; 0759665229,0757228705,067578658
''Hakika moyo wangu unaonekana kuangamia kwani pale nilipopenda sipendwi labda kuna mwenzangu kashapendwa''

OLIETER kipenzi kwanini umeamua kuutesa moyo wangu kiasi hiki,unanifanya mudamwingi nijikunyate kama kifaranga kwenye baridi kali la ukungu mithiri ya giza aliye sahaulika na mama yake wakati wa mawindo ya chakula.
haya ni baadhi ya maneno yanayonijia kichwani mwangu mara kwa mara tangu nikufahamu olieter kipenzi, kwani hakika amani imetoweka moyoni mwangu hata nikilala badala ya kuota ndoto nzuri juu yako imekuwa kinyume nafikiria labda kunaweza kukapatikana kisasi ili niweze kulipa ili tugawane mateso haya, kwani mawazo kwa sasa juu yako ni zaidi ya mtihani wa taifa kwaajili ya maisha yangu hapa duniani.
Kiukweli tangu nikufahamu olieter nilitokea kukupenda bila ya kuchamba na kuchambua yatakayo tokea hapo mbeleni, nilidhani labda ndo ulikuwa mwisho wa mahangaiko yangu ya kutafuta mwenza kutokana na ugumu wa maisha ya sasa hadi kumpata mwenzako anaekupenda na kukujali ni shughuli kwelikweli lakini fikra zangu zilienda tofauti na fikra zako.
ukaribu wetu mama nadhani ndio sababu yangu kudanganyika kirahisi, kwani tulikaribiana kwa kila kitu ukianzia makazi,elimu,umri sawia,utani mwingi, na upendo uliojidhihirisha kati yetu hata majirani wakajisemea kweli wamependana haya yote yalinifanya nijione nimefika na kupata kumbe nimefikwa na kupatwa.
Nakumbuka siku yangu ya kwanza kuonana mimi na wewe moyo wangu ulipwita pwiiii japo kimoyomoyo nikijisemea hakika bahati ya mtende imewadia,Ujasiri wangu ndio ulipelelekea haya yanayo nikuta leo hii, mana nilijikuta natoa mneno matamu nikidhani natoa mahala salama kumbe ndio naizika furaha yangu.
Hukuwa na kinyongo mtoto wa watu uliyapokea niliyokwambia jambo ambalo lilinitia jeuri kwano mwitikio wako chanya ulinifanya nione kuwa nimekwishafika sihitaji tenda kuendelea mbele, lakini kumbe sasa nilipoteza muda wangu bure.
Nayakumbuka maneno yako ya mwanzo yale ya siku za mwanzo wa mazoea yetu yalikuwa ni yenye kunitia hamasa kwa sanamoyoni mwangu na kujiona naweza kuwa nawewe maishani mwangu kipenzi OLIETER.Kama sijakosea nakumbuka baadhi ya maneno uliyokuwa ukiniambia kama,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,ITAENDELEA


Endelea kufuatilia simulizi yetu sehemu ya pili ni hapo baadaye saa moja na nusu hapahapa GODYNEWS TZ.


AHSANTE 
@the blogger

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya