SERIKALI KUTAKA KUFUTA MANISPAA YA SONGEA

Serikali imesema kuwa itaifuta manispaa ya Songea na kuvunja baraza la Madiwani kwa mujibu wa sheria kwa sababu ya kukithiri kwa migogoro inayokwamisha miradi ya maendeleo ya wananchi,kauli hiyo imetolewa na Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa ambapo amesema serikali haipo tayari kuona wananchi wanakosa huduma muhimu kwa sababu ya maslahi ya madiwani wachache.

Akiongea na watumishi wa manispaa ya songea waziri mkuu Kasimu Majaliwa ametoa onyo kali kwa madiwani wakiongozwa na meya wa manispaa hiyo Abduli Mshaweji kuacha marumbano na migogoro isiyokuwa na tija vinginevyo ataifuta halmashauri na kuvunja baraza la madiwani.

Aidha amemtaka mkurugenzi wa manispaa ya Songea kusimamia sheria pale anapoona meya anakataa kusaini mikataba kwa sababu zisizo za msingi amtumie naibu meya kwa kuwa naye anayo mamlaka ya kusaini mikataba.

Amegusia miradi ya maji,majengo na barabara kuwa imekwama kwa sababu ya migogoro ya madiwani na baadhi ya wakuu wa Idara kwa maslahi yao binafsi, amewaonya wakuu wa idara.

Aidha kuhusu mgogoro wa maeneo ya uwekezaji EPZA kata ya Mwengemshindo kutolipwa malipo ya fidia Zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa miaka kumi amewaagiza watendaji wanaohusika na uwekezaji kuthaminisha upya maeneo hayo kwani sheria inasema usipolipa ndani ya miaka miwili uthamishaji unapaswa kuanza upya na kama hawatafanya hivyo wananchi wataendelea na shughuli zao.

Waziri mkuu kasimu majaliwa alikuwa na ziara ya siku moja ya kuongea na watumishi na kutembelea eneo lenye mgogoro la Mwengemshindo,kutoka Songea MKOANI Ruvuma mimi ni Geofrey Nilahi

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).