Airtel ni Mali ya TTCL kwa 100% – Rais Magufuli

Airtel ni mali ya TTCL kwa 100% – Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wanaotoa takwimu zisizo kuwa sahihi wachukuliwe hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo ambayo vinatokea mara kwa mara hapa nchini.


Mhe. Magufuli amesema hayo leo wakati akiweka jiwe la Msingi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuungana na Serikali kuhamia mkoani humo ambako ndio makao makuu ya nchi.

''Natoa onyo kwa watu wote wanaotoa takwimu zisizokuwa sahihi wachukuliwe hatua kali za kisheria ambazo tumezitunga wenyewe na kuzisaini, ili kukomesha matatizo ambayo yanatokea kutokana na kutolewa kwa takwimu zisizo rasmi, yoyote anayehitaji kujua takwimu afike sehemu husika ya chombo hicho,'' amesema.



Kifungu namba 37 cha sheria ya takwimu, kifungu kidogo cha 3 hadi 5 kinaruhusu mtu au taasisi yoyote inayotoa takwimu isiyokuwa sahihi afungwe miezi 6 hadi miaka 3 pamoja na faini ya milioni moja  hadi milioni kumi au vyote kwa pamoja.

Magufuli pia amesisitiza ofisi ya Takwimu kuendelea kutoa takwimu sahihi kwa lengo la kuwapa taarifa makini wananchi ambazo zitasaidia kuonesha hatua za maendeleo. 

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).