KUMEKUCHA : Simba wamfungashia virago JOSEPH OMOG.




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Klabu ya Simba na kocha wake Mkuu Joseph Omog wameamua kwa pamoja Kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano ya ya pande zote mbili
Klabu ya Simba inamtakia Kila la Kheri kocha Omog kwenye Maisha yake nje ya Simba.
Kwa wakati huu timu itakuwa chini ya Kocha msaidizi Massoud Djuma na itaendelea na mazoezi hapo kesho. Ambapo siku ya Jumatatu itapumzika kwa ajili ya sikukuu ya Christmas na Jummane kuingia kambini kwa ajili ya Safari kuelekea Mtwara.
Pia kwa niaba ya Uongozi, benchi la ufundi na wachezaji wote tutumie nafasi kuomba radhi sana mashabiki wetu na wanachama wote kutokana na matokeo ya Jana ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, ila tuwaombe muwe wavumilivu katika kipindi hiki ili kufikia malengo yetu.
Mwisho klabu inawataka kheri ya sikukuu ya Noeli na mapumziko mema ya wikiendi.
Imetolewa na Haji Manara
Mkuu wa Habari Simba SC

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya