Takribani watu 200 wameripotiwa kufariki Kwa Kimbunga
FILIPINO: Takribani watu 200 wameripotiwa kufariki, huku maelfu ya wengine wakiachwa bila makazi baada ya kimbunga kilichopewa jina la Tembin kuikumba sehemu ya Kusini ya nchi hiyo.
-
Ufilipino inakumbwa na wastani wa vimbunga 20 kwa mwaka vinavyoharibu mali na kusababisha vifo vya watu.
-
Wiki iliyopita watu 46 waliuawa na kimbunga eneo la katikati mwa nchi hiyo na mwaka 2013 kimbuga kikubwa cha Haiyan kiliua watu karibia 8,000 na kuwaacha wengine zaidi ya 200,000 bila makazi.
Comments
Post a Comment