HATIMAYE SIMBA DEAL DONE!!! Yafanikiwa kumsajili Asante KWASI
- Get link
- X
- Other Apps
Klabu ya soka ya Lipuli FC imetoa taarifa kuwa tayari imepokea ofa ya shilingi milioni 25 kutoka Simba kwaajili ya kumsajili beki Asante Kwasi raia wa Ghana.
Taarifa iliyotolewa leo na idara ya habari ya Lipuli FC imeeleza kuwa tayari Simba imekamilisha taratibu zote za usajili zinazohitajika na hivyo kuanzia sasa Asante Kwasi anaweza kutangazwa kuwa mchezaji halali wa Simba SC.
Tayari uongozi wa Lipuli FC umeliandikia barua shirikisho la soka nchini TFF, kuthibitisha kufikia makubaliano ya kumwachia mlinzi huyo mwenye mabao matano, akakitumikie kikosi cha vinara wa ligi Simba SC.
Simba ambayo jana jioni imeondolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho imekuwa ikihaha kupata saini ya Kwasi ili kuziba nafasi ya Method Mwanjali ambaye ameachwa.
Dirisha dogo la usajili linafungwa leo saa sita usiku baada ya kuwa wazi kwa takribani mwezi mmoja na nusu. Awali lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Disemba 15 kabla ya kuongezwa muda hadi leo kutokana na mtambo wa usajili wa FIFA kupata hitilafu
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment