Michezo miwili ya FA yaahirishwa kisa leseni za wachezaji


Michezo miwili ya kombe la Azam Sports Federation Cup (FA Cup) imeshindwa kuchezwa jijini Dar es Salaam kwa sababu ya wachezaji kukosa leseni za kufanyia kazi hivyo mechi hizo zimeahirishwa hadi TFF itakapotoa mwongozo juu ya suala hilo.

Mchezo wa Abajalo vs Tanzania Prisons (uwanja wa Uhuru) umeshindwa kuchezwa baada ya wachezaji zaidi ya watano wa Abajalo kugundulika kuwa hawana leseni za kuwaruhusu kucheza mashindano.

Mchezo mwingine ambao haujachezwa kwa sababu ya wachezaji kukosa lesini ni kati ya Mvuvumwa dhidi ya JKT Ruvu (uwanja wa Azam Complex).

Katibu mkuu wa Tanzania Prisons Havinitishi Abdallah amethibitisha kwamba mchezo huo haujachezwa na wao wanasubiri kusikia TFF inasemaje kwa kile ambacho kimetokea kwenye mchezo wao dhidi ya Abajalo.

“Hatujacheza kwa sababu wachezaji kama saba wa Abajalo hawakuwa na leseni, tunasubiri kusikia kutoka TFF kwa sababu wao ndio wanazitoa, baada ya hapo ndio tutajua tuseme nini lakini kwa sasa hatuwezi kuongea chochote.”

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya