Rais Magufuli Awatoa Hofu ya Ajira Wanaosomea Ualimu

Rais Magufuli Awatoa Hofu ya Ajira Wanaosomea Ualimu


Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Disemba 14, 2017 akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu nchini Tanzania (CWT) amezungumzia juu ya ajira za ualimu na kusema kuwa ajira zipo hivyo walimu wanafunzi wanaosomea ualimu wasiwe na mashaka.

Magufuli amesema hayo wakati akifungua Mkutano Kuu wa Chama Cha Walimu nchini (CWT) na kusema kuwa serikali yake inatoa ajira kwa walimu na kudai awali walisitisha zoezi la kuajiri kutokana na uhakiki wa vyeti feki kwa madai ya kuwa waliogopa wasije kurudia kosa la kutoa ajira kwa watu ambao hana sifa hizo.
"Mwaka huu pekee tumeajiri walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati wapatao 3,462 walimu wengine wapatao elfu kumi na tano na mia moja thelathini na tano wakiwepo wa Sayansi wanatarajiwa kuajiriwa wakati wowote baada ya vyeti vyao kuhakikiwa, kwa hiyo kuna walimu wa masomo mbalimbali tunahakiki vyeti vyao ili tusiingie kwenye matatizo ambayo tuliyaona na baada ya kuhakiki vyeti vyao wataajiriwa" alisema Rais Magufuli
Aidha Rais Magufuli amewatoa wasiwasi walimu wanafunzi na kusema kuwa ajira zipo nyingi hivyo wakimaliza masomo yao watapata kazi bila tatizo
"Nataka niwahakikishie mnaosoma hapa chini ya mwalimu Profesa. Kikula ajira zipo na nyinyi tena bahati nzuri tumeamia hapa hapa Dodoma mtakuwa unatufuata tu mnatuambia sisi tunahitaji ajira na hasa kwa sababu shule zinaongezeka, idadi ya wanafunzi inaongezeka hivyo ajira ya walimu lazima iongezeke, lakini pia tunaendelea kupanua wigo wa kuzalisha walimu" alisisitiza Rais Magufuli

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya