DR. Shika ATANGAZA NIS YA KUOA
Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amefunguka na kutangaza nia ya kutaka kuoa endapo atapata mwanamke ambaye anamuhitaji.
Dkt. Shika amesema kuwa kwa sasa hana mpango wowote wa kurudiana na wanawake ambao amezaa nao watoto nchini Tanzania bali anatafuta mwanamke mwingine mpya ambaye atamuoa
"Nikimpata anayenihitaji na mimi nikamuhitaji nitaoa , saizi nipo tu kwanza nasubiri ila siyo kama sina mpenzi kwani wapenzi huwa hawakosekani mnakutana, mnapendana lakini mjue kuwa mpenzi na mke ni watu wawili tofauti. Siwezi kabisaa kurudiana na wazazi wenzangu kwani hicho kipindi kimepitwa na wakati saizi nataka mpya" alisema Dkt. Shika
Mbali na hilo Dkt. Shika amesema kuwa hawezi kuhama katika nyumba ambayo anaishi kwa kuwa anaishi bure kwenye nyumba hiyo hivyo ataondoka endapo atapata nyumba yake ila kuondoka na kwenda kupanga ni jambo ambalo hataliweza na kuwa hata huyo rafiki aliyempa nyumba hiyo atamshangaa
Comments
Post a Comment