Mwanamke Mkenya Aweka Kambi Nyumbani Kwa DIAMOND PLATNUMZ
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanamke mmoja raia wa Kenya ameripotiwa kuweka kambi nje ya nyumba ya staa wa Muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania, Diamond Platinumz, akidai kuwa hapewi matunzo ya mtoto aliyezaa na msanii huyo.
Mwananmke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Pensheni Salama anayedai kuwa raia wa Kenya aliripotiwa kukesha yeye na mtoto wake nje ya nyumba ya Diamond, ikiwa ni jitihada za kutaka kumpata msanii huyo.
Mama Pensheni alipohojiwa alieleza kuwa ni kwa muda mrefu sasa amekuwa akimtafuta Diamond bila mafanikio, na amekuja nyumbani kwake baada ya kusikia kuwa mzazi mwenzake na Diamond, Zari Hassan yupo nchini Tanzania, hivyo anaweza kumsaidia kwani naye ni mwanamke kama yeye.
Disemba 19, Walinzi wa mtaa anaoishi Diamond baada ya kumkuta Mama Pensheni akiwa amelala nje ya nyumba ya msanii huyo, walimpeleka kwa Mjumbe wa Mtaa kwa ajili ya kumhoji.
Mjumbe wa Mtaa wa Mivumoni, Christina Chilumba alipotafutwa na kuhojiwa alikiri kuwa ana taarifa za ujio wa mwanamke huyo na kueleza kuwa Mwenyekiti wa mtaa ndiye mwenye taarifa zaidi kumuhusu.
“Ni kweli huyo mwanamke alikuja na kulala na mtoto wake pale getini kwa msanii huyo baadaye alipelekwa ustawi wa jamii lakini zaidi mtafuteni mwenyekiti ambaye kwa sasa yuko kikaoni yeye atawaeleza kwa undani zaidi,” alisema Christina.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mvumo, Deo Kamugisha alieleza kuwa ni kweli sungu sungu wanaolinda mtaa huo walimkuta mwanamke huyo akiwa amelala nje ya nyumba ya Diamond na kumuhoji.
“Kundi la sungusungu wanaolinda mtaa wetu usiku, walikuwa wanapita maeneo ya nyumbani kwa msanii huyo wa Bongo Fleva na kumkuta mwanamke akiwa na mtoto wake mchanga akiwa amelala getini na walipomhoji ilibidi waniamshe ili nije kumsikiliza” alisem Kamugisha.
“Nilitoka usiku huo wa saa nane na tukamhoji ambapo mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Pansheni Salama alieleza kuwa ametokea Kenya na amefika Dar kwa ajili ya kumletea mtoto msanii huyo kwani amezaa naye.” aliongeza.
Kamugisha alieleza kuwa tofauti na mwanamke huyo, wapo watu wengine wengi ambao wamekuwa wakija kumtafuta msanii Diamond bila mafanikio na kuishia mikononi mwa mwenyekiti wa mtaa, jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa mtaani hapo.
“Kiukweli tunapata usumbufu mkubwa sana na msanii huyo kwani tunatumia hela zetu kuwarudisha makwao watu wanaomfuata bila mafanikio kwani amekuwa hasikilizi watu, namshauri tu angewasikiliza watu au kuwa na sehemu yao maalum ili kutupunguzia mzigo tunaokumbana nao,” alisema mwenyekiti.
Hata hivyo mwanamama huyo, amewahi kuripotiwa kudai kuwa mtoto huyo alizaa na msanii Ali Kiba, lakini alipohojiwa aliikiri kuwa kwa wakati ule hakuweza kuwatofautisha Ali Kiba na Diamond, ila baada ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha kwa kina ana uhakika na amejiridhisha kuwa mtoto huyo ni wa Diamond.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment