CANNAVARO. Bado ninamatimaini na Manji

Wakati mabosi wa Yanga wakiwa kwenye mipango ya kumpa mwekezaji klabu yao, beki na nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kuwa kama akipewa Yusuf Manji, basi wapinzani wao watawatambua.

Kauli hiyo, aliitoa hivi karibuni mara baada ya klabu hiyo kutangaza kuwa kwenye mipango ya muundo mpya wa uendeleshaji wa klabu hiyo katika kuleta mabadiliko.

Yanga kama wakifanikiwa hilo, basi watakuwa wameungana na Simba ambao wenyewe tayari wamempatia klabu hiyo bilionea, Mohamed Dewji ‘Mo’.

Cannavaro alisema kwanza anaupongeza uongozi wa timu hiyo kwa maamuzi waliyoyafanya ya kumpa mwekezaji katika kuhakikisha klabu yao inafikia mafanikio mazuri zaidi ya hapo walipo.

Cannavaro alisema, amesikia tetesi za Manji kurejea klabuni akiwa kama mwekezaji, hivyo kama taarifa hizo zikiwa ni kweli, basi watafanya vizuri katika mechi zijazo za Ligi Kuu Bara kutokana na morali ya wachezaji kuongezeka.

Aliongeza kuwa, katika kipindi chake akiwa mwenyekiti kabla ya kuomba kupumzika katika timu, alifanikisha mengi na kati ya hayo ni kuchukua mara tatu mfululizo ubingwa wa ligi na kuifikisha timu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Nimesikia tetesi za Manji kurejea Yanga lakini kama mwekezaji lakini sina uhakika, nikwambie kuwa kama akirejea tena katika timu, basi niamini watatutambua wapinzani.

“Kama unavyojua uendeshaji wa timu unahitaji fedha nyingi, hivyo kurejea kwake kutasaidia baadhi ya vitu kwenda vizuri ikiwemo kuuchukua tena ubingwa wa ligi kuu kwa mara nne mfululizo.

“Ninaamini morali ya wachezaji itaongezeka kwa kasi kubwa kwa maana ya kuipambania timu zaidi ya hivi tunavyoipambania timu yetu,” alisema Cannavaro


Tazama video jinsi Zanzibar walivyo umizwa na matokeo yao na kenya 

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya