Yanga yaifunga mdomo Simba



Ushindi wa Yanga wa mabao mawili 2-0 dhidi ya Reha FC imedhihirisha kuwa timu hiyo iliingia uwanjani ikiwa na ari ya kupata ushindi.

Timu hiyo ya Jangwani ilifanya mashambulizi kadhaa ambayo wapinzani wao walijitahidi kufanya hivyo pia, lakini umakini wa makipa wa pande zote uliwafanya kuingia kipindi cha pili kwa kila timu bila kuona lango la mwenzake.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru umedhihirisha kuwa timu za Ligi Daraja la Pili siyo za kubeza kutokana na kuonyesha soka la kuvutia.

Wiki hii Simba ambao walikuwa mabingwa mtetezi, walifungwa na Green Warriors timu ya Ligi Daraja la Pili mchezo ulioisha kwa kupigiana mikwaju ya penalti 4-3.

Yanga imefanikiwa kuvuka hatua raundi ya tatu ya michuano hiyo ya Kombe la FA kwa mabao yaliyowekwa wavuni na Amissi Tambwe na Pius Buswita

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya