Aina 10 ya wanawake wanaopendwa na wanaume


WENYE MSIMAMO
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.

WAPENDA USAWA
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.

WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.

MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.

WA WAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.

WANAOJITEGEMEA 
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.

WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.

MARIDADI 
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano.

WANAORIDHIKA
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.

WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya