Simba tupo tayari kuwavaa warriors kesho


Klabu ya Simba mapema leo imefanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya kesho jioni kuwavaa wapinzani wao, Green Warriors kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam, katika mchezo wao wa kujiwinda na Kombe la Shirikisho maarufu kama FA.

Simba ambayo imeweka kambi yake ndani ya Sea Scape Two iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, imehitimisha mazoezi yake hayo na kwamba kesho itashuka katika dimba hilo kusaka nafasi ya kutetea ubingwa wa kombe hilo ambalo walilitwaa msimu uliyopita kwenye mchezo wa fainali yao ulikutanisha dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Akizungumza na mtandao huu baada ya mazoezi yao kukamilika, Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Omog, amesema kuwa vijana wake wapo tayari kwa mapambano, zaidi anasubiria hiyo kesho ifike ili wakamilishe dhamira yao kupata ushindi.

“Tumemaliza mazoezi salama hivyo hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutujalia uzima, zaidi sasa tunaelekea kambini kwa ajili ya kupumzika ili kesho tuweze kushindana ili tupate ushindi kwenye mchezo huo muhimu, najua nakutana na timu mabayo siifahamu sana hivyo natumaini mchezo utakua mgumu sana kwetu,” alisema Omog.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya