Posts

Showing posts from 2017

DR. Shika ATANGAZA NIS YA KUOA

Image
Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amefunguka na kutangaza nia ya kutaka kuoa endapo atapata mwanamke ambaye anamuhitaji. Dkt. Shika amesema kuwa kwa sasa hana mpango wowote wa kurudiana na wanawake ambao amezaa nao watoto nchini Tanzania bali anatafuta mwanamke mwingine mpya ambaye atamuoa "Nikimpata anayenihitaji na mimi nikamuhitaji nitaoa , saizi nipo tu kwanza nasubiri ila siyo kama sina mpenzi kwani wapenzi huwa hawakosekani mnakutana, mnapendana lakini mjue kuwa mpenzi na mke ni watu wawili tofauti. Siwezi kabisaa kurudiana na wazazi wenzangu kwani hicho kipindi kimepitwa na wakati saizi nataka mpya" alisema Dkt. Shika Mbali na hilo Dkt. Shika amesema kuwa hawezi kuhama katika nyumba ambayo anaishi kwa kuwa anaishi bure kwenye nyumba hiyo hivyo ataondoka endapo atapata nyumba yake ila kuondoka na kwenda kupanga ni jambo ambalo hataliweza na kuwa hata huyo rafiki aliyempa nyumba hiyo atamshangaa

CHIRWA AREJEA Baada ya kufanikiwa kuikwepa simba

Image
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia habari zetu kila dadika, na pia fuatilia magazeti ya leo juma pili kwa taarifa zaidi

MAGAZETI YA LEO TAR 31/12/2017

Image

Airtel ni Mali ya TTCL kwa 100% – Rais Magufuli

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wanaotoa takwimu zisizo kuwa sahihi wachukuliwe hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo ambayo vinatokea mara kwa mara hapa nchini. Mhe. Magufuli amesema hayo leo wakati akiweka jiwe la Msingi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuungana na Serikali kuhamia mkoani humo ambako ndio makao makuu ya nchi. ''Natoa onyo kwa watu wote wanaotoa takwimu zisizokuwa sahihi wachukuliwe hatua kali za kisheria ambazo tumezitunga wenyewe na kuzisaini, ili kukomesha matatizo ambayo yanatokea kutokana na kutolewa kwa takwimu zisizo rasmi, yoyote anayehitaji kujua takwimu afike sehemu husika ya chombo hicho,'' amesema. Kifungu namba 37 cha sheria ya takwimu, kifungu kidogo cha 3 hadi 5 kinaruhusu mtu au taasisi yoyote inayotoa takwimu isiyokuwa sahihi afungwe miezi 6 hadi miaka 3 pamoja na faini ya milioni moja  hadi milioni kumi au vyote kwa pamoja. Magufuli pia amesisit...

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

Image
  Mahusiano yoyote yale huhitaji mtu mwenye uvumilivu, imara, mkweli na muwazi lakini hivi vyote vikishindikana basi, mahusiano hayo huingia doa. Watu kuwa na wapenzi wawili wawili huenda ikawa sijambo geni, lakini ni jambo geni pale mwezi wako akilifanya. Matatizo haya yamekuwepo kwa miaka mingi, lakini sidhani kama yatakuja kuzoeleka, maana kila mmoja hapa anahitaji upendo wa dhati na wakwake tuu, usio na kugawana na mtu mwingine. Vitabu vya dini vinasisitiza upendo ulio mmoja katika mahusiano yaliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, 'tuliheshimu hili'. Katika makala hii inayolenga kukuonyesha dalili za mwenzi wako kutoka nje ya mahusiano, kwa kiasi kikubwa itakusaidia wewe kuwa sehemu sahihi. Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mpenzi wako anamahusiano nje ya ndoa au urafiki wenu. 1.  Mmekuwa wawazi kwa muda sasa, yani mwenzi wako amekuwa akishea na wewe mambo mbalimbali ya siku nzima, ghafla anaanza kuchelewa kurudi kutoka kazini, na akirudi hakuambii ali...

Mwanamke Mkenya Aweka Kambi Nyumbani Kwa DIAMOND PLATNUMZ

Image
  Mwanamke mmoja raia wa Kenya ameripotiwa kuweka kambi nje ya nyumba ya staa wa Muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania, Diamond Platinumz, akidai kuwa hapewi matunzo ya mtoto aliyezaa na msanii huyo. Mwananmke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Pensheni Salama anayedai kuwa raia wa Kenya aliripotiwa kukesha yeye na mtoto wake nje ya nyumba ya Diamond, ikiwa ni jitihada za kutaka kumpata msanii huyo. Mama Pensheni alipohojiwa alieleza kuwa ni kwa muda mrefu sasa amekuwa akimtafuta Diamond bila mafanikio, na amekuja nyumbani kwake baada ya kusikia kuwa mzazi mwenzake na Diamond, Zari Hassan yupo nchini Tanzania, hivyo anaweza kumsaidia kwani naye ni mwanamke kama yeye. Disemba 19, Walinzi wa mtaa anaoishi Diamond baada ya kumkuta Mama Pensheni akiwa amelala nje ya nyumba ya msanii huyo, walimpeleka kwa Mjumbe wa Mtaa kwa ajili ya kumhoji. Mjumbe wa Mtaa wa Mivumoni, Christina Chilumba alipotafutwa na kuhojiwa alikiri kuwa ana taarifa za ujio wa mw...

MAGAFULI APATA TUZO HII

Image
Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii. Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya. Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao. Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi. "Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarish...

Mahusiano Kabla ya Ndoa Kati ya Msichana na Kijana wa Kiume.

Image
Asanteni tena kwa kujumuika nasi hapa katika ukurasa huu unaolenga kuwafungua watu katika maswala mbali mbali ya kijamii, yanayokwamisha maendeleo ya watu pamoja na kusambalatisha mahusiano ya watu. Leo tunaangalia mambo ya kuzingatia kabla ya kuingia katika ndoa, na hapa wengi huenda nikaenda tofauti nao, lakini ni jukumu langu kuelimisha jamii na sio kuifurahisha tuu. Kila mtu anafahamu neno mahusiano ya kirafiki kati ya jinsia mbili tofauti. Kabla ya kuingia katika ndoa, lazima ufanye urafiki na mtu unayetaka kumuoa au kuolewa naye, ili uweze kubaini tabia na mwenendo wake kama unaendana na wakwako, au anamatatizo gani ya kiafya au kiukoo pia. Tumekuwa tukikimbilia kufanya mapenzi ili kupima uwezo wa injini kama inahimili safari na kusahau usukani wa gari, kwani gari haliwezi kukufikisha pale unapotaka kwenda bila ya kuwa na uskani (staring). Kwa wachumba na wasio wachumba yani Girlfriend na Boyfriend, kama kweli unampango wa kumuoa au kuolewa, ni vyema usiendekeze kufanya mape...

Sifa15 Zinazomfanya Mwanamke Kumpenda Mwanaume.

Image
Pengine watu wengi wamekuwa wakitafuta ni jinsi  gani wanaweza kupendwa na wasichana au wanawake. Niwazi kabisa kila mwanamke anachaguo lake kwa mwanaume ampendae.Huenda ukawa unavigezo kibao lakini akapenda mweyevigezo vichache. Vifuatavyo ni vigezo 15 ambavyo wasichana wengi hupenda kutoka kwa mwanaume. 1. Kujiamini 2. Mcheshi 3. Mwenye utashi 4. Anayetoa msaada unapohitajika 5. Anaetunza siri 6. Mwenye kujithamini 7. Mwenye malengo / makini  8. Mwenye mawazo mapana  9. Muwazi na mkweli   10. Anayeridhika       11. Aliyeshupavu na jasiri 12. Mwenye huruma 13. Anaesamehe 14. Hadhi na heshima 15. Hisia ya uadilifu.

Mbinu 15 za Kumtongoza Mwanamke Akakupenda Daima

Image
Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote. Hapa kunanjia 15 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo ; 1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla. 2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa ukizungumzia. 3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza nae huku akikupatia majibu yasiyo na hisia zozote za mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo kama kwa bahati mbaya uko nae karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa katik...

Kufanya Mapenzi Ofisini Kunavyoadhiri Mtu Kisaikologia

Image
Kula nanasi kunahitaji nafasi, wengi wamekuwa wakishawishika kufanya mapenzi katika eneo la kazi kutokana na kupendana ama vishawishi mbali mbali kutoka kwa kinadada hususani katika mavazi. Sina maana mbaya ninaposema kina dada kwasababu wengi wao ndio wanaoacha sehemu zao nyeti wazi, kwamfano kuvaa nguo fupi sana na kuvaa vitop vinavyoonyesha sehemu kubwa ya maziwa wazi. Kwa asilimia miamoja watu wengi wanaofanya mapenzi kwa kuiba katika maeneo kama ya ofisini huwa hawakumbuki kuvaa kinga kutokana na mihemumko mikali na ya haraka kuliko kawaida wanayokuwa nayo kwa wakati huo. Ni vyema kujihadhali ma mihemuko hii kwani madhara yake ni makubwa. Mihemuko hii huwakumba watu wote hata ambao wako katika ndoa, kutokana na vishawishi vya mwenzake basi anajikuta amezama katika saa za kazi. Tabia hii ikifanyika mara tatu huanza kuwa kama sehemu ya majukumu ya wezi hawa wa mapenzi. Kinadada wanaovaa nguo fupi katika makazi ya watu huenda wakawa wanafanya hivyo kwasababu ya fasheni, wengine ...

Lukuvi, Ummy Mwalimu watajwa tena

Image
Siku 6 kabla ya kufunga mwaka 2017, wasomaji na wafuatiliaji wa habari kupitia mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), wametoa maoni wakiwataja mawaziri watano wa Serikali waliofanya vizuri katika maeneo wanayoyasimamia. Wametoa maoni hayo takriban wiki moja baada ya gazeti hili kufanya tathmini ya utendaji wa mawaziri watano. Katika orodha hiyo, mawaziri wawili wameingia katika makundi yote mawili ambao ni William Lukuvi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ummy Mwalimu anayeisimamia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto. Wananchi wametoa maoni hayo kupitia swali lililoulizwa kwenye akaunti za MCL za mitandao ya kijamii za Instagram, Facebook na Twitter. Swali hilo lililoambatana na picha ya Rais John Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri lililisema, “Ni waziri gani katika Serikali ya Rais Magufuli ambaye amekuvutia kwa utendaji wake mwaka huu? Kwa nini? Toa maoni yako.” Mbali ya Lukuvi na Ummy, mawaziri w...