Yanga Kuwakosa wachezaji hawa Mchezo wa Kesho Dhidi ya Azam FC

Yanga Kuwakosa  Kuukosa Mchezo wa Kesho Dhidi ya Azam FC


Wachezaji saba wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wataukosa mchezo wa kesho unaotarajiwa kuchezwa dhidi ya Azam FC katika dimba la Azam Complex kutokana na sababu mbalimbali walizokuwa nazo.


Hayo yamebainishwa leo na Afisa Habari wa klabu hiyo Dismas Ten na kuwataja wachezaji kuwa ni Yohana Mkomola, Thaban Kamusoko, Amisi Tambwe, Abdallah Shaibu, Donald Ngoma pamoja na Patongonyani ambao wote hawa ni majeruhi huku Pius Buswita akiwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Azam FC ni wachezaji saba pekee ndio watakaokosa mchezo huo kama nilivyosema lakini kila kitu kimekamilika. Tunaiheshimu sana Azam kwani wamekuwa na msimu mzuri wanapata matokeo ndani na nje ya uwanja wao wa nyumbani ila ata sisi Yanga SC tupo vizuri na tunatarajia kupata matokeo kwenye mchezo wa kesho", alisema Dismas Ten.

Azam FC kesho itakuwa inamkaribisha Yanga SC katika dimba lao la nyumbani ambapo mchezo huo utachezwa majira ya 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya