V Money AJA NA KITU MPYA KWA AJILI YA MASHABIKI WAKE

Diva wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee 'Vee Money' ameendelea kuwa na wiki ya kihistoria ambayo ilianza kwa kuzindua albamu yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake na wadau wengine wa muziki nchini siku ya Jumatatu.

Leo Vanessa amezindua programu ‘app’  yake mpya ya simu ya VEE  MONEY ambayo inapatikana bure kupitia ‘Google Play store’ na ‘Apple store’.

Programu hii ambayo imetengenezwa na kampuni ya masuala ya teknolojia ya Marekani, Converge Media, ni sehemu ambayo mashabiki wa Vanessa watakuwa wanapata maudhui ya kipekee ya Vanessa kama vile; nyimbo, video, picha, na kuona kurasa zake za kijamii.

‘Kwanza natoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea albamu yangu kwa mikono miwili, na sasa natumaini app hii itazidi kutuweka karibu’ alisema Vannesa.

Vanessa atakamilisha wiki yake ya kihistoria kesho kwa kuweka sahihi katika album zake tukio ambalo litafanyika eneo la Mlimani City Mall kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya