Kamanda Muslim Kushuhudia Mtanange wa Azam na Yanga Kesho

Kamanda Muslim Kushuhudia Mtanange wa Azam na Yanga  Kesho


Klabu ya soka ya Azam FC imemtangaza Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslim, kuwa ndiye mgeni rasmi kwenye mchezo wake wa kesho dhidi ya Yanga.


Akiongea leo mbele ya waandishi wa habari msemaji wa klabu hiyo Jaffary Idd amemtaja Kamanda Muslim kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ambao utawashuhudia mabingwa watetezi Yanga wakicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Azam Complex.

Aidha Jaffary pia amesema pamoja na kuandika barua ya kuomba kubadilishwa kwa mwamuzi aliyepangwa kuchezesha mchezo huo Israel Nkongo, lakini hadi sasa bado wanamtambua kama mwamuzi kwani hawajapata taarifa yoyote ya kukubaliwa au kukataliwa kwa ombi lao.

Bado tunamtambua Israel Nkongo kama mwamuzi wa mchezo wetu wa kesho lakini tunamuomba atende haki'', amesema Jafarry.

Kwa upande wake kocha msaidizi wa mabingwa hao wa mapinduzi Idd Cheche, amesema wanaiheshimu klabu ya Yanga lakini wamejiandaa kuhakikisha wanawapa raha na ladha ya soka mashabiki wa soka watakaojitokeza sambamba na kusaka alama tatu muhimu. 

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya