CHIRWA ATUA KIMYA KIMYA USIKU


Mzambia wa yanga Obrey Chirwa amerejea nchini ijumaa juzi usikuakitokea kwo , huku uongozi ukisisitiza kuna ishu wanaiweka sawa kabla hajajiunga na wenzake Zanzibar.

Taarifa za awali zinasema kwamba mchezaji huyo mchezaji huyo alikuwa amesusa akitaka kumaliziwa chake alichokuwa akidai kwenye fungu la usajili, ingawa zipo taarifa kuwa alishindwa kurejea Dar es salaam kwa wakati baada ya Yanga kushindwa kumtumia tiketi.

mchezaji huyo alionekana kwenye picha tofauti akijihusisha na kilimo alipokuwa kwao huku wenzie wakiendelea kupiga mzigo.
Katibu mkuu wa Yanga Chaeles Bonface Mkwasa aliliambia spot xtra kuwa ''Chirwa amerejea alipokuwa ameenda baaada ya kupata matatizo ya kifamilia, kwahiyo muda wowote atakapo malizana na uongozi atakwenda Zanzibar kuungana na timu.
kuna baadhi ya nmambo yake yalikuwa hayaja kaa sawa ambayo siwezi kuyasemea lakini yakiisha kuwa sawa ataenda Zanzibar kuungana na wenzake.

Alipo ulizwa kuhusiana na fedha za usajili ambazo Chirwa anadai hiyo Mkwasa alisema
''suala hilo kwa sasa siwezi kulizungumzia ila ninachoweza kusema kwa sasa tunadaiwa na wachezaji wengi na taratibu za kuwalipa zinaendelea.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya