“Singida United Mmetuletea Kitu Kipya Katika Soka la Bongo”-Shaffih Dauda
Bila shaka kila mtu ni shahidi juu ya picha ya mafanikio waliyoibeba Singida United ndani na nje ya uwanja kwa muda mfupi ambao wamerejea ligi kuu Tanzania bara.
Singida United ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 nyuma ya Simba na Azam ambao wana pointi 26 katika nafasi ya kwanza na ya pili. Wamecheza mechi 12 hadi sasa wameshinda mechi sita, sare tano na kupoteza mchezo mmoja.
Walichokifanya kwenye Mapinduzi Cup kila mmoja amekiona, katika mechi sita walizocheza wamepoyeza mchezo mmoja tu wa nusu fainali dhidi ya Azam mchezo ambao uliwafanya waondolewe kwenye mashindano hayo ambayo walishiriki kwa mara ya kwanza katika historia.
Imetoa wachezaji watano (5) pamoja na kocha bora wa kikosi cha mashindano ya Mapinduzi msimu huu lakini katika mechi sita walizocheza, wachezaji wa Singida United walitajwa kuwa man of the match katika mechi tano.
Siku za nyuma kulikuwa na mechi za aina tatu ambazo zilikuwa zinaonekana zina mvuto, kwa maana kwamba mechi ya Simba vs (timu nyingine), Yanga vs (timu nyingine) na Yanga vs Simba hizo ndio zilikuwa mechi zinazofuatiliwa sana na wadau wa soka na kuonekana zina mvuto, lakini inapofika mechi za (timu nyingine) vs (timu nyingine) hakuna watu wanaofuatilia kwa hiyo matokeo yake ilijenga ushindani wa timu mbili ambazo zilikuwa zinapokezana.
Walipoingia Azam wakaongeza kifurushi cha nne, kwa maana ya kwamba, Simba vs (timu nyingine), Yanga vs (timu nyingine), Simba vs Yanga halafu iliyoongezeka ikawa Simba vs Azam na Yanga vs Azam lakini wigo ukaendelea kuzizunguka Simba na Yanga.
Ushindani wa Azam ulipoingia kati yao (Simba na Yanga) ukaongeza mzuka lakini kwa bahati mbaya Azam pamoja na ubora wake mpaka leo bado hawana wigo mpana wa mashabiki kitu ambacho kinaongeza thamani ya profile ya klabu ukiachilia mbali kubeba mataji mbalimbali lakini bado haina wafuasi wengi.
Kwa hiyo inapokuja mechi ya Azam vs (timu nyingine) bado mechi inakosa mzuka mkubwa, utamu wa mechi ya Azam vs Simba au Yanga unatokana na ushindani ambao Azam wamekuja nao lakini ujio wa Singida United ni changamoto nyingine na tofauti.
Uwezo wa kumchukua kocha Hans van Pluijm ni mara chache sana kuona kocha mwenye ubora kama wa Hans kwenda kufundisha timu za nje ya Dar kwa sababu ni mara nyingi makocha wote wakali wanaishia Dar, wakitoka hapo wanarudi makwao.
Kitendo cha Singida United kumchukua Hans kiliwashtua wengi na kuanza kujiuliza kuhusu nguvu ya klabu hiyo, wakati wanajiuliza juu ya hilo, mfungaji bora wa Rwanda Danny Usengimana akatua pale, Singida wakaonesha jeuri ya kumchukua Deus Kaseke ambaye aliivimbia Yanga impe mkataba mnono kama hawataki yuko tayari kuondoka na sio kwamba aliachwa, walishindwa kukubalia lakini Singida ilifikia dau la mchezaji huyo na kumchukua.
Namna wanavyoendesha mambo yao, idadi ya wadhamini walioingia mikataba na Singida United kabla hata ligi kuanza ikafanya watu waanze kufuatilia kwa karibu kuona uwekezaji uliofanywa itakuwaje uwanjani, kwa bahati nzuri hadi sasa hawajawaangusha watu. Kwa hiyo sasa hivi Singida United wamengia kwenye kundi la timu zinazopigania ubingwa (Singida United, Azam, Yanga, Simba na Mtibwa) licha kwamba Mtibwa huleta changamoto mwanzoni lakni mwishoni mwa msimu wanakimbia.
Kutokana na mazingira yalivyo sasa hivi, mechi zenye mvuto kwenye ligi zimeongezeka, zamani zilikuwa Simba vs (timu nyingune), Yanga vs timu nyingine) na Simba vs Yanga, baadae walivyokuja Azam zikaongezeka kwa hiyo ujio wa Singida United nao umeongeza changamoto kwa sababu mechi ya Singida dhidi ya timu nyingine inafuatiliwa, halafu mechi ya Azam na timu nyingine pia inafuatiliwa kwa sababu mashabiki wanataka kujua nini kitatokea huko ili kupata picha ya ushindani kwenye mbio za ubingwa wa ligi.
Kwa sasa ligi imetanuka na ushindani umeongezeka ukilinganisha na zamani, ushindani huu uachwe hivihivi ili timu inayostahili kuchukua ubingwa ichukue isijekufika sehemu yakafanyika magumashi na mizengwe ya kubadilisha mambo.
Zamani inapotajwa timu ya taifa, kuna wachezaji wakiitwa watu wote wanabaki kimya kwa sababu hakuna wengine zaidi ya hao walioitwa, lakini ligi ikiwa na ushindani ikitajwa timu ya taifa halafu hakuna jina la Habib Kiyombo, hakuna jina la Feisal Salum ‘Fei Toto’ watu lazima watahoji kwa sababu kuna wachezaji wengi wanye sifa za kuitwa na hiyo ndio inazua mijadala hata ukimuuliza kocha atakupa sababu kwa nini amemwita huyu akamwacha yule.
Kocha atakwambia kutokana na mechi tunayokwenda kucheza, tunahitaji kuwa na mchezaji wa aina fulani kulingana na mazingira ya mchezo lakini nimemuacha yule si kwa sababu ni mbaya bali hatofiti kwenye mechi ijayo. Kwa hiyo ushindani ukiwa mkubwa kwenye ligi inakuwa ni faida kwa nchi na si vilabu pekee

Comments
Post a Comment