AISHI MANULA AUAGA UKAPELA RASMI
Golikipa wa Simba na Taifa Stars Aishi Manula, amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi Bi. Aisha.
Ndoa hiyo imefungwa leo Jumamosi Januari 6, 2018 Mkamba mkoani Morogoro.
Manula hayupo Zanzibar ambako klabu yake inashiriki kombe la Mapinduzi na alikuwa na ruhusa maalum kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kufunga ndoa.
Leo usiku Simba itacheza dhidi ya Azam katika mchezo wa Kundi A michuano ya Mapinduzi wakati huo Manula akisherekea ndo yake
Comments
Post a Comment