LWANDAMINA KUREJEA NA DAWA YA SIMBA
MASHABIKIwa Yanga bado wana shaka na nguvu ya benchi lao la ufundi chini ya makocha wasaidizi, Shadrack Nsajigwa na Noel Mwandila, hasa kutokanana uwezekano wa kukutana na watanizao Simba kwenye nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, lakini kocha wao Mzambia, George Lwadamina ameshusha presha.
Lwandamina yupo kwao Zambia alipokwenda kumzika mwanaye, Mofya aliyefariki dunia mwezi uliopita, lakini atarejea nchini usiku wa kesho Jumamosikisha kwenda Zanzibar kuongeza nguvu kwenye kombe la Mapinduzi ambalo bingwa mtetezi wake ni Azam.
Yanga imekuwa nawakati mgumu mbele ya Simba hasawakati wapinzani wao hao walipokuwa wakinolewa na Mkameruni, Joseph Omog ambaye alisitishiwa mkataba wake mwezi uliopita baadaya kuvuliwa ubingwawa FA na timu dhaifu ya Green Warriors.
Katika kipindi cha Omog, Simba iliifunga Yanga mara moja katika Ligi Kuu na kuishindakwa mikwaju ya penalti kwenye Mapinduzi Cup naNgao ya Hisani mwaka jana, hukumichezo mingine miwili ikimalizika kwa sare jambo ambalo Lwandaminahataki litokee tena nandiyo sababu amechukua uamuzi wa kutua nchini fasta.
Kwa namna hesabu za Mapinduzi zilivyokaa, Simba naYanga zinaweza kukutana nusufainali ama fainali, lakini dili hilo huenda likatibuliwa na Azam na Singida United ambazo zinaonekanakuwa na ushindani mkubwa katika mashindanohayo.
Kama Yanga itamaliza juu kwenye kundi lake na Simba kumaliza nafasiya pili, wababehao watakutana nusu fainali lakini mambo yakiwatofauti itabidi wapambane iliwakutane fainali.
Katika mechitatuza mashindano ambazo Lwandamina amezikosa, Yanga imepotezamabao 2-0 kwa Mbao FC, lakini imeshinda kwa idadi kama hiyo dhidi ya Reha na kuifunga Mlandege2-1.
Taarifaza uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata kutoka ndani ya Yanga ni kwamba Lwandamina ambaye alirudi kwao Zambiakwa ruhusa maalumu kisha kukutana na msiba wa mwanaye wa kiume Mofya, anatua nchini kesho usiku.
Lwandamina atakutana na uongozi wa klabu hiyo kabla ya kwendaZanzibar ambako atakutakikosi chake kimebakisha mchezo dhidi ya Singida United utakaopigwa siku ya Jumatatu ikiwa niwa mwisho wa hatua ya makundi na utakaoamua kamawa nakutana na Simba au ala!!
Wakati huo huo, leo Ijumaa Shirikisho la SokaTanzania (TFF) litachezesha droo ya Kombe la FA kubaini timu zitakazokutana kwenye raundi ya tatu ya michuano hiyo. Timu 13 za Ligi Kuu isipokuwa timu zilizotolewa ambazoni Mbeya City, Simba na Lipuli zitashiriki katika droo hiyo.
NSAJIGWA AFUNGUKA
Katika hatua nyingine, Nsajigwa ameliambia Mwanaspoti kuwa ataendelea kumpa nafasi kipa chipukizi, Ramadhani Kabwili katika mechihizo za Mapinduzi ilikumjenga kiushindani.
Nsajigwa alisema kipa huyo nimzuri lakini alikuwa hapatinafasi ya kucheza mara kwa mara hivyo sasa niwakati wake kujituma na kutengeneza jina.
KABWILI ALIDAKA KWENYE MCHEZO WA KWANZA DHIDI YA MLANDEG E.
“Alicheza vizuri katika mechiya kwanza, tutampa nafasiiliaendelee kuonyesha kilealichonacho. Hii nimichuano yenye mechinyingi, hivyo kila mmojaanaweza kucheza,” alisema.
Comments
Post a Comment