Nay wa Mitego Aendelea Kuwa na Balaa la Kukataliwa na Mademu...Mrembo Nini Nae Amkana



Msanii wa muziki Bongo, Nini amefunguka kuhusu ukaribu wake na Nay wa Mitego.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Niwe Dawa’ alioshirikiana na Nay ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper huyo.

Kauli ya Nini anakuja baada ya hapo awali kuwepo taarifa kuwa sababu ya kutimuliwa MJ Record ni kuwa na mahusiano na Nay.

“Sina mahusiano ya kimapenzi na Nay, halafu hata kama ningekuwa nayo, kiupande wangu I don’t real think hiyo ni sababu ambayo ingeweza kumfanya yeye afanye kile alichokifanya,” amesema.

“Seriously sidhani kama mahusiano ya kimapenzi yanaweza kuathiri muziki, sina uhakika may be according to me navyofikiria lakini sidhani kama hiyo it can be specific reason,” amesisitiza.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya