JE YANGA ATAPIGA WAZENJI WOTE


Yanga tayari imetinga hatua ya nusu fainali ya kombe la mapinduzi baada ya akushinda michezo mitatu mfululizo na leo jumapili saa 2:15 usiku itavaana na zimamoto katika uwanja wa Amani zanzibar.
mchezo huo utakuwa ni mwendelezo wa hatua ya makundi baada ya Yanga kucheza mechi tatu walizo shinda zote dhidi ya JKU 1-0,JANG'OMBE 2-0 na MLANDEGE 2-1.

Endapo Yanga itashinda mchezo huo itaandika rekodi ya kuzifunga timu zote za Zanzibar ambazo wako nazo pamoja kwenye kundi lake.

kutokana ana matokeo hayo Yanga imefikisha alama tisa ikiwa na mechi mbili mkononi.Baada ya mchezo huo Yanga itakamilisha ratiba ya makundi hapo kesho jumatatu itakapokuwa ikivaana na aSingida united inayofundishwa na kocha wa zamani wa timu hiyo Hans Van Der Pluijk.

Yanga ambayo ipo kwenye kundi B ambalo lina timu kama Singida Utd,T.Jang'ombe,JKU,Mlandege na Zimamoto.

AJIBU ATOA SIRI.
Ibrahim Ajibu amefunguka kuwa kujituma uwanjani kwa bidii ndiyo imekuwa siri na yenye kufanya vizuri katika michuano hii.
''nashukuru mungu timu yangu imekuwa ikifanya vizuri lakini upande wangu siri kubwa mimi kufanya vizuri ni kujituma kwa n=bidii nikiwa uwanjani na kuuiisaidia timu kupata matokeo mazuri,alisema'' AJIBU ambaye aliibuliwa na Goran Kupunovic kwenye kikosi cha vijana cha Simba

CHANZO.SPOTI XTRA.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya