TFF YAMFUNGIA MAISHA KIONGOZI HUYU.

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia maisha kutojishughulisha na mchezo wa mpira wa miguu Dunstan Mkundi ambaye alikuwa Msimamizi wa Kituo cha Mtwara.

Mkundi amefungiwa kwa kosa la kushindwa kuwasilisha fomu ya mapato ya mchezo kati ya Ndanda FC na Simba uliofanyika Desemba 30, mwaka jana Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara ndani ya saa 48 kama kanuni inavyotaka.

Kamati hiyo iliyokutana Januari 18 imeanisha kuwa kosa la kushindwa kuwasilisha fomu ya mapato ya mchezo ambayo ni kinyume na Kanuni ya 32 (2) Kanuni za Ligi Kuu toleo la 2015.

Aidha, Mkundi pia ameshindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusu utata wa fomu mbili zilizowasilishwa zikionyesha utofauti wa mapato kwa kiasi cha shilingi Milioni tatu laki saba kumi elfu(3,710,000).

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara Kizito Mbano, amefungiwa kutojihusisha na shughuli za Mpira wa Miguu kwa kipindi cha miaka Mitano(5) kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha kanuni za maadili TFF toleo la 2013

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya