OKWI NA NIYONZIMA KUMBE LAO NI MOJA TU

Emmanuel okwi amewaambia mashabiki wa simba kuwa licha ya yeye kutokuwa sehemu ya kikosi kwa sasa katika michuano ya Mapinduzi lakini kwa jinsi anavyoona kwene Azam Tv hakuna wa kuwazuia kunyakua ndoo.

Okwi hatofautiani na Hruna Niyonzima ambaye amepewa kazi pevu ya kujifua bichi jijini Dar es salaam lakini anaamini kuwa kombe litakwenda Simba kwa kuwa sasa vijana wameamua kufanya kazi.
Okwi mwenye mabao nane kwenye ligi kuu bara ameshindwa kuwa sehemu ya wachezaji wa Simba wanaoshiriki mapinduzi kutokana na kubaki kwao uganda ambako anaendelea na matibabu ya enka.

Akizungumza na spoti xtra Okwi ambaye anasherekea sikukuu yake ya kuzaliwa Desemba 25 kila mwaka,''mimi sipo ndani ya timu kwa sasa lakini nikwambie tu kuwa bado sijaona timu ambayo inaweza kuisimamisha Simba, sababu ukitazama wachezaji ambao wapo, wana viwango vya hali ya juu sana na uzoefu mkubwa wa kufanya vyemakatika michuano hiyo, na imani yangu ni kwamba Simba lazima wachukue ubingwa huo wa Mapinduzi hata kama sipo, alisema Okwi.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya