SIMBA yazidi kujiweka pazuri baada ya kuifumua Kagera Sugar bao 2-0
Klabu ya soka ya Simba imelipa kisasi dhidi ya Kagera Sugar baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo uliomalizika jioni hii uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Simba ilibidi kusubiri hadi dakika ya 69 kuweza kupata bao lake la kwanza kupitia kwa kiungo Said Ndemla ambaye alipata pasi kutoka kwa Shiza Kichuya dakika 10 baadaye Simba kupitia kwa John Bocco wakaandika bao la pili.
Matokeo ya leo yanaifanya Simba SC kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikifikisha alama 32 katika michezo 14 na kuishusha Azam FC yenye alama 30.
Katika mchezo mwingine uliopigwa leo kati ya Singida United dhidi ya Majimaji FC, timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1 hivyo Singida kubakia katika nafasi ya 5 ikiwa na alama 24, nyuma ya Yanga na Mtibwa Sugar zenye alama 25.
Msimu uliopita April 22, Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar na kukwamishwa mipango yake ya ubingwa

Comments
Post a Comment