Binti mwenye uvimbe begani afariki dunia....Waziri Ummy Amlilia



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema amesikitishwa na kifo cha msichana Marim Sandalu (17) aliyekuwa na uvimbe begani.


Mariam ambaye ni mkazi wa Masasi mkoani Mtwara, amefariki dunia leo alfajiri akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI).

 

Binti huyo ambaye alitakiwa kufanyiwa upasuaji Muhimbili mwaka mmoja uliopita wakati huo uvimbe ukiwa bado mdogo, alitoweka baada ya kwenda katika tiba za asili kabla ya kurejea hospitalini hapo Januari 3 mwaka huu, baadaye kuhamishiwa katika taasisi hiyo.


Waziri Ummy amesema inasikitisha kwani msaada wa Watanzania haukuweza kuokoa maisha yake.


“Tutaongeza jitihada zaidi kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwahi hospitalini kufanyiwa uchunguzi na kuzingatia maelekezo ya madaktari wanayopewa ikiwamo kuanza matibabu mara moja na si kwenda kukaa nyumbani na mgonjwa,” amesema Waziri Ummy ambaye hivi karibuni alimtembelea Mariam hospitalini kumjulia hali.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya