Wasafi Tv na Redio Kuvuka Mipaka, Diamond Ataja Nchi hii
Wakati watu wakisubiria ujio wa Wasafi Tv na Redio, Diamond Platnumz ameeleza mipango ya kupeleka vyombo hivyo vya habari kuonekana na kusikika nje ya nchi.
Muimbaji huyo akizungumza nchini Rwanda ambapo ameenda kwa ajili ya kuzindua biashara zake amesema kuna mipango ya kuhakikisha Wasafi Tv na Redio zinafika nchini humo.
“Na pia tupo katika harakati za kuhakikisha kwamba ziwe na uwezo wa kufika hadi nchini Rwanda kwa namna moja au nyingine endapo tutamalizana na vyombo vya sheria,” amesema.
Ameongeza kuwa lengo la Wasafi Fm na Tv ni kuona kwa namna gani vyombo vya habari vinavyoongezeka vinasaidia wasanii kukua kwani kuna wasanii wanajua kuimba lakini hawapati nafasi.
Comments
Post a Comment