Emmanuel Eboure Ataka Kujinyonga Kisa Mapenzi

Emmanuel Eboure Ataka Kujinyonga Kisa Mapenzi


Nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboure ameweka bayana jambo lililomfanya afikirie kujinyonga kutokana na matatizo yanayomkabili.

Nyota huyo aliweka bayana suala la kutalakiana na mkewe, Aurelie ambaye mahakama kuamuru umiliki wote wa mali zitahamishiwa kwa mwanamke huyo ni mambo ambayo amesema yanamvuruga akili.

Eboue alisema kwamba amevumilia kuwa nje ya soka kwa takribani mwaka mzima lakini kubwa linalokoroga ni matatizo yaliyotokana na talaka na mkewe, pia anakabiriliwa na majonzi baada ya kufiwa na ndugu zake wawili wa karibu.

Alisema mambo hayo yameharibu mfumo mzima wa maisha yake jambo amablo limemfanya kuishi kama ombaomba, huku akiweka bayana kwamba hakuwahi kuwa na elimu ya kutunza fedha zake vyema.

Mkongwe huyo mwenye miaka 34, aliitumikia Atsenal tangu mwaka 2004 hadi 2011 kabla ya kuhamia Uturuki ambako alikuwa akiichezea klabu ya Galatasaray.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya